Kwa ufupi:
Soya ni zao linalopatikana katika mimea ya jamii ya mikunde ambayo inahusisha mazao mengine kama maharage, njugu mawe, mbaazi, kunde, fiwi, dengu na choroko. Zao hili linaaminika kuwa asili yake ni Asia ya mashariki. Mbegu ya mazao hutofautiana kwa ukubwa, nyingine zikiwa ndogo sana na nyingine zikiwa kubwa kiasi na vile vile rangi kuanzia nyeusi hadi rangi inayokaribia manjano.