xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | TANZANIA FORESTRY RESEARCH INSTITUTION (TAFORI) | |
dc.date.accessioned | 2022-04-12T11:44:35Z | |
dc.date.available | 2022-04-12T11:44:35Z | |
dc.date.issued | 2019-06-15 | |
dc.identifier.issn | 0856-496 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/594 | |
dc.description.abstract | Siku ya nyuki duniani ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutunza viumbe wanaochavusha mimea hususan nyuki, kutambua madhara ambayo yanakabili viumbe hao na kujua mchango wake kwa maendeleo endelevu. Nyuki ni mdudu muhimu sana katika mfumo ikolojia na maisha ya mwanadamu, kwani huchavusha asilimia 70 ya mimea inayohudumia asilimia 90 ya watu duniani. Nyuki wana mchango mkubwa katika maisha ya mwanadamu, hivyo jamii inatakiwa kuwatunza. Kwa kutambua umuhimu wa nyuki, Baraza la Umoja wa Mataifa (“The United Nations General Assembly”) lilipitisha azimio kuwa kila tarehe 20 Mei iwe Siku ya Nyuki Duniani. Azimio hilo liliridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuatia pendekezo la Solvenia la Desemba 2017 la kuifanya tarehe 20 Mei kuwa siku ya nyuki duniani. Chimbuko la siku ya nyuki duniani lilitokana na Bwana Anton Jansa aliyezaliwa siku ya tarehe 20/5/1734. Bwana Anton alikuwa mwalimu na mwasisi wa ufugaji nyuki duniani. Alifafanya ufugaji wa nyuki kitaalamu, aliandika vitabu na kufundisha ufugaji nyuki nchini Slovania. Bwana Anton aliwathamini sana nyuki na moja ya kati ya vitabu vyake alivyoandika ni“Bees are a type of fly, hardworking, created by God to provide man with all honey and wax” maana yake nyuki ni wadudu wachapakazi walioumbwa na Mungu kumpatia mwanadamu mahitaji yake yote ya asali na nta. Hivyo, sherehe za kuadhimisha siku ya nyuki duniani hufanyika kila mwaka tarehe 20 Mei kwa heshima ya Bwana Anton Jansa | en_US |
dc.description.sponsorship | JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MALIASILI TAASISI TA UTAFITI TANZANIA | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) | en_US |
dc.subject | Miche ya matunda | en_US |
dc.subject | Kubebesha vikonyo | en_US |
dc.subject | Kupanda miti | en_US |
dc.subject | Kloni za mikaratusi | en_US |
dc.subject | Ufugaji Nyuki | en_US |
dc.subject | Utafiti wa ufugaji | en_US |
dc.subject | Miche bora ya matunda | en_US |
dc.title | Jarida la TAFORI | en_US |
dc.title.alternative | Maadhimisho ya pili ya siku ya nyuki duniani | en_US |