Kwa ufupi:
Siku ya nyuki duniani ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa
kutunza viumbe wanaochavusha mimea hususan nyuki, kutambua madhara ambayo
yanakabili viumbe hao na kujua mchango wake kwa maendeleo endelevu. Nyuki ni mdudu
muhimu sana katika mfumo ikolojia na maisha ya mwanadamu, kwani huchavusha asilimia
70 ya mimea inayohudumia asilimia 90 ya watu duniani. Nyuki wana mchango mkubwa
katika maisha ya mwanadamu, hivyo jamii inatakiwa kuwatunza.
Kwa kutambua umuhimu wa nyuki, Baraza la Umoja wa Mataifa (“The United Nations
General Assembly”) lilipitisha azimio kuwa kila tarehe 20 Mei iwe Siku ya Nyuki Duniani.
Azimio hilo liliridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuatia pendekezo la
Solvenia la Desemba 2017 la kuifanya tarehe 20 Mei kuwa siku ya nyuki duniani. Chimbuko
la siku ya nyuki duniani lilitokana na Bwana Anton Jansa aliyezaliwa siku ya tarehe
20/5/1734. Bwana Anton alikuwa mwalimu na mwasisi wa ufugaji nyuki duniani. Alifafanya
ufugaji wa nyuki kitaalamu, aliandika vitabu na kufundisha ufugaji nyuki nchini Slovania.
Bwana Anton aliwathamini sana nyuki na moja ya kati ya vitabu vyake alivyoandika ni“Bees
are a type of fly, hardworking, created by God to provide man with all honey and wax”
maana yake nyuki ni wadudu wachapakazi walioumbwa na Mungu kumpatia mwanadamu
mahitaji yake yote ya asali na nta. Hivyo, sherehe za kuadhimisha siku ya nyuki duniani
hufanyika kila mwaka tarehe 20 Mei kwa heshima ya Bwana Anton Jansa