Kwa ufupi:
Kilimo cha Giligilani (coriander) ni mradi mkubwa unaojitosheleza na zao hili huchukua muda mfupi toka kuotesha hadi kuvuna. Giligilani hutumika kama kiungo cha chakula katika mapishi mbalimbali kama nyama, supu au mchuzi. Giligilani hulimwa katika maeneo mengi ya Tanzania hususani mikoa ya Mbeya, Iringa na Arusha.