Kwa ufupi:
Timu ya watafiti wenye ujuzi na taaluma mbalimbali kutoka mradi wa HALI ukishirikiana na wafugaji wanaoishi
Kusini-Mashariki mwa Hifadhi ya taifa Ruaha waliweza kutambua na kuorodhesha magonjwa ambayo yanashambulia
mifugo yao na hivyo kuandaa mwongozo huu kuhusu afya za mifugo. Abigail Ahmed, wa mtandao wa Afya Moja
na mbunifu wa michoro kutoka Chuo Kikuu cha Nebraska-Lincoln, ndiye aliyebuni na kuchora michoro katika
mwongozo huu na Kelly Kretchmer alichangia muonekano wa sehemu ya mbele ya mwongozo huu.
Tunawashukuru wafugaji wote kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Tanzania kwa ushirikiano wao na mrejesho
waliotoa wakati wa kuandaa mwongozo huu. Vile vile tunawashukuru wafanyakazi wa mradi wa HALI na washirika
wetu kwa kupitia na kutoa mawazo yao wakati wa kuandaa mwongozo huu kama vile: Deana Clifford, Christopher
Gustafson, Mathias Matandala, Jonna Mazet, Jesca Mlawa, Hilda Mrema, Goodluck Paul, Zikankuba Sijali, Robert
Sumaye, na David Wolking.
Mwongozo huu umeandaliwa kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Feed the Future Livestock and Climate
Change Innovation Lab katika Chuo Kikuu cha Colorado na Idara ya utafiti wa kilimo ya Chuo Kikuu cha NebraskaLincoln.