Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na
Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), na Chuo Kikuu cha Kilimo
chaNorway (NLH), kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa
Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania.
Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000,
unagharamiwa na Serikali ya Norway na Serikali ya Tanzania.
Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malenqo ya
mradi na kuimarisha uhusiano na wakulima, watafiti na wataalarnu
wa ugani ni kupanga utaratibu na kuwawezesha wakulima
kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Ziara
hizo za kimafunzo zina madhumuni yafuatayo:
1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa ugani
ili kujifunza zaidi kutoka kwa wakulima wenzao na hata
wakulima wabunifu kwa lengo la kufanikisha kilimo na
ufugaji
2. Kutambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima
wadogowadogo
3. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya
kilimo na mifugo.
Chapisho hili linawasilisha ripoti ya ziara ya wakulima
wadogowadogo waliotoka Kanda ya Mashariki na Nyanda za Juu
Kusini iliyofanyika Aprili 2005. Wakulima hawa waliwatembelea
wenzao wa Mkoa wa Kllirnanjaro, wilaya za Hai, Moshi Vijijini na
Rombo.