Kwa ufupi:
Chapisho hili linawasilisha Mwenendo wa Warsha ya Tatu ya Wakulima wa Kanda ya
Mashariki kuhusu uimarlshaji wa mahusiano yaliyopo baina ya wakulima wa ma.zao na
wafugaji. Warsha ilifanyikakatika Kituo eha Don Bosco Mjini Songea tarehe 26 hadi 29
Novemba 2001.
Warsha hii ni moja ya warsha ambazo zimepangwa kufanyika kama shughuli muhimu za
kuutekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa
Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi Septemba 2000,
unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD), na
unatekelezwa na Chuo Kikuu eha Sokoine eha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya
Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu eha Norway eha Kilimo. Warsha hizi zina
madhumuniyafuatayo:
I. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo na washika dau
wengine ill kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji kushirikishwa pande
zote kwa lengo la kufanikishakilimo.
2. Kuchambuana kuainishamatatizo yanayowakabillwakulima wadogowadogo.
3. Kudadisi illkutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele zaidi.
4. Kushirikikatika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo.
Kamati ya Utekelezaji wa Mradi inatarajia kuwa ehapisho hili litakuwa 1amanufaa kwa
wadau mbalimbali, na mapendekezo yaliyotolewa na washiriki wa warsha yatachangia
katikajuhudi za kuimarishauhakika wa chakula nchini.