Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana
na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula (MAFS), pamoja
na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza
Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa
Wakulima Wadogo Wadogo Tanzania.
Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano
kati ya Wakulima, Watafiti na Wagani. IIi kufikia lengo hili,
mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima
kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda.
Makala hii inawasilisha mafunzo yatokanayo na ziara
iliyofanyika Septemba 2002. Ziara hii iliwashirikisha
wakulima na washauri wa wakulima kutoka Kanda ya
Mashariki ikijumuisha wilaya za Kilosa, Handeni, Pangani,
Mkuranga na Morogoro na kanda ya Nyanda za Juu Kusini
ikiwajumuisha wakulima na wagani kutoka wilaya za Mbeya,
Mafinga, Njombe, Mbinga na Mbozi ambao walitembelea
wakulima wa wilaya ya Arumeru, Arusha walioshiriki katika
rnradi wa SCAPA. Makala hii pia inapatikana katika lugha ya
kiingereza.