Kwa ufupi:
Karafuu ni zao linalotokana na mkarafuu, ingawa karafuu hazimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa muhimu sana kwa maisha ya binadamu.Mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyinginezo katika karne ya 19. Miche ya mikarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Indonesia, mashariki ya mbali mwaka 1818.
Mikarafuu inastawi zaidi Visiwani vya Unguja na Pemba ambapo katika miaka 30 iliyopiata Zanzibar ilikuwa inazalisha asilimia 80 ya karafuu zote zinazohitajika duniani ambapo uchumi wake ulitegemea sana zao la karafuu.