Kwa ufupi:
Tikitimaji au tikiti-maji ni tunda la mtikiti-maji lenye maji na nyama ambalo huchangia kutoa ngaziya juu ya vitamini, madini n.k. Matikitimaji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hiyo inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama matango, maboga na maskwash Kuna vitu ambavyo umekuwa ukividharau au kuona havifai kabisa unapokuwa unakula vyakula aina fulani haswa ikija kwenye ulaji wa mbegu au maganda ya matunda kama zabibu, maboga n.k. Kusoma makala hii itakusaidia kufahamu kiundani kuhusu faida za kiafya za mbegu za tikiti maji na namna ya kutumia mbegu hizo ili kupata faida zake.