Kwa ufupi:
Nyanya ni moja ya mazao ya mbogamboga muhimu Tanzania
hususan katika wilaya ya Muheza. Zao la nyanya humwongezea
mkulima kipato na kuboresha lishe ya mlaji. Pamoja na faida
zake hizi. zao la nyanya ni la msimu na linakabiliwa na matatizo
mcngi likiwemo la kuharibika haraka mara tu baada ya kuvunwa.
llali hii pia humlazimisha mkulima auze nyanya zake haraka na
kwa bei ya chini ambayo humpunguzia kipato. Wakulima wa
Muheza kama walivyo wakulima wa sehemu nyingine Tanzania
hawasindiki nyanya zao kwa sababu hawana ujuzi huo. Kijitabu
hiki kimetayarishwa ili kumsaidia mkulima au mtu yeyote
mwingine kusindika pesti ya nyanya na kuhifadhi katika chupa
kwa ajili ya matumizi ya baadaye.