Kwa ufupi:
Ili kupata chakula chenye madini ya kutosha na ya kufana wataalamu hushauri tule matunda na mboga mboga kwa wingi. Na mojawapo ya vyakula hivi ni tunda au mmea aina ya beetroot kama unavyofahamika zaidi kwa kimombo.
Beetroot ni zao ambalo jina lake kibaiolojia huitwa Beta vulgaris. Na zao hili tunda lake hujiunda katika mizizi kama kitunguu. Beetroot ni muhimu sana kwa kuongeza damu na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Inaweza kuliwa kama ilivyo baada ya kuvunwa au ikatengenezwa juice na ikatumika vizuri kabisa.
Lakini pia majani yake yanalika kama spinach. Kwa ukuaji bora wa mimea hii inahitaji mvua ya kutosha. Pia hukubali vyema katika udongo wenye rutuba na wa kitifutifu. Udongo wa mfinyanzi ambao ukikauka unapasuka husababisha tunda kuwa na umbo ambalo sio zuri kibiashara.