Kwa ufupi:
Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) litasafirisha mafuta kutoka kwenye kituo
cha mafuta, kilichopo Wilayani Hoima, nchini Uganda, kuelekea kwenye kituo cha kuhifadhia na kituo cha kupakia mafuta kwenye meli kwenda nchi za nje, vilivyopo kwenye rasi ya Chongoleani, kaskazini mwa mji wa Tanga katika Pwani ya Afrika Mashariki, Tanzania.
Athari zinazoweza kutokana na mradi, faida na hasara kwa uchumi, jamii na mazingira nchini Tanzania zimefanyiwa tathmini na kuelezwa kwa kina katika nyanja mbalimbali zilizodhaniwa kuwa za thamani na muhimu katika jamii (kwa mfano, kudumisha njia za kujikimu). Mbinu za kuepuka au kupunguza athari zilizo mbaya zimeelezwa na baada ya hatua hizo kutekelezwa, athari zinazofikiriwa kubakia pia zimeelezwa.
Taarifa ya Tathmini ya Athari za kimazingira na kijamii imeandaliwa kwa kuzingatia: