Kwa ufupi:
Mchaichai kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia
kama dawa ya mbu. Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana aida kubwa kiafya. Mafuta vya mchaichai hutumika katika viwanda vinavyotengeza pafyumu na sabuni. Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupamban ana athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Wengine huamini kuwa mchaichai huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya
matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.
Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa.