Kwa ufupi:
MABADILIKO YA TABIA NCHI na hali ya hewa isiyotabilika kwa pamoja huchangia changamoto kubwa kwa wakulima wadogo wadogo katika eneo la Afrika Mashariki.Vi Agroforestry inafanya kazi na wakulima pamoja na asasi za wakulima kuongeza ufahamu wao wa mazingira, kuwasaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza matumizi ya nishati mbadala/endelevu na pia kuzuia na kupunguza athari za majanga asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.Usimamizi Endelevu wa Ardhi ya Kilimo (SALM) ni mbinu zinazotumiwa na wakulima katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza tija katika uzalishaji kwenye kanda mbalimbali za kilimo ikolojia. Mbinu hizi pia zinaweza kutumiwa katika maeneo ya mijini kwa mfano bustani za mbogamboga, mbinu zinazohusu ukulima, nishati mbadala na usimamizi wa maji na maji taka. Mwongozo huu umeweka mbinu mbalimbali ambazo mkulima anaweza kuzitumia kama hatua ya kweli katika kuongeza tija na faida hata kwa vizazi vijavyo hasa kutokana na ufahamu wa hali ya hewa na tabia ya nchi inayobadilika duniani kote na kuathiri uzalishaji wa tija