Kwa ufupi:
Sekta ya kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za nje ya nchi. Sekta hii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote nchini na kuzalisha mazao ya chakula na biashara. Mazao makuu ya chakula ya aina ya wanga yanayozalishwa ni pamoja na mahindi, mpunga nk. Mazao hayo na mengine ndiyo yanayochangia Taifa kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 100. Pamoja na kujitosheleza kwa chakula na kuchangia katika uchumi wa Taifa, takriban mazao yote hayo yamekuwa yakizalishwa kwa tija ndogo kwa maana ya kiasi cha mazao yanayozalishwa kwa eneo. Aidha, uzalishaji umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya mazao hayo kuzalishwa katika maeneo yaliyo nje ya ikolojia yake ya asili na ukosefu wa pembejeo bora ikiwemo mbolea.
Wakulima wengi kwenye kilimo cha mahindi na mpunga nchini wamekuwa wakikumbana na changamoto kwenye matumizi ya mbolea, ambapo wanatumia mbolea za mazoea mengine ambazo husababisha mavuno kuwa hafifu shambani. Lakini ujio wa mbolea ya MiCROP inayozalishwa na kuuzwa na kampuni ya Yara imekuja kuwa mkombozi kwa wakulima hawa kwani sasa wataondokana na kupata mavuno machache ya gunia saba kwa hekali na kuongezeka hadi kufikia gunia 30 shambani ama zaidi.