Kwa ufupi:
Zao la mpunga liliingizwa nchini Tanzania miaka mingi iliyopita na wafanya biashara wa kutoka Mashariki ya Kati na India. Katika ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika zao hili hulimwa kwa wingi nchini Madagascar na Tanzania
inafuatia.Nchini Tanzania, zao la mpunga hulimwa katika mikoa yote na
ni la pili kwa umuhimu wake kama zao la chakula baada ya mahindi. Asilimia 60% ya Watanzania waishio mijini hula wali, chakula kinachotokana na zao hili.
Ingawa zao la mpunga huzalishwa kwa wingi nchini, kiwango cha mavuno yanayopatikana kwa ekari au hekta moja bado ni cha chini sana ukilinganisha na nchi nyingine zinazolima zao hili. Hii inatokana na wakulima wengi kutokuwa na elimu ya zao la mpunga na kutozingatia kanuni za kilimo bora cha zao
hili.