Kwa ufupi:
Mwaka 2005/2006 Tanzania inakabiliwa na upungufu
inkuwa wa chakula. Sababu kubwa ya upungufu huo ni
hah ya ukame ulioikumba nchi yetu.
Hata hivyo tatizo hilo la upungufu wa chakula lisingckuwa
kubwa kiasi hicho iwapo wananchi kwa ujumla
wangekadiria sawa sawa kiasi cha chakula
wanachohilaji na kukihifadhi wakati wa mavuno.
Ukadiriaji wa mahitaji ya chakula katika kaya ni jambo
la muhirnu katika kuhakikisha kuwa familia hasa za vijijini
zinakuwa na chakula cha kutoshelcza mahitaji ya mwaka
mzima.
Kaya ikifahamu mahitaji yake itaweka mipango thabiti
ya uzalishaji kulingana na mahitaji ya chakula na matumizi
mengine kama vile kuuza, kutoa zawadi, kufanya sherehe
na shughuli mbalimbali za mila na'desturi.
Wakati wa kukadiria kiasi cha mazao ya kuhifadhi katika
kaya ni muhirnu kuzingatia idadi ya watu katika kaya,
utaalam wa kuhifadhi, vyombo au sehemu ya kuhifadhia
na matumizi mengine .