Kwa ufupi:
Kwa muda mrefu wazee wetu wamekuwa wakitegemea kilimo.
Mahitaji yao yote yamekuwa yakitokana na mashamba yao na misitu.
Hawakuwa na shida kubwa ya chakula au kuni Leo hii mabadiliko mengi yametokea. Watu wameongezeka sana. Sasa hivi huwezi kufungua shamba mahali popote tu; kila shamba lina mwenyewe. Sio ajabu siku hizi kusikia kesi nyingi zinazohusu mashamba na mipaka. Sasa hivi huwezi kulima kilimo cha kuhamahama au kupumzisha shamba kama walivyofanya wazee.
. Siku hizi rutuba ya udongo imepungua sana; matokeo yake mavuno nayo yamepungua. Sehemu nyingine watu wanatumia mbolea kupita kiasi na kuharibu udongo. Sasa hivi upatikanaji wa kuni umekuwa wa tabu. Katika sehemu za milimani kama Mgeta matatizo hayo ni makubwa zaidi.
Wakulima wa huko kila siku wanayashuhudia matatizo haya.