Kwa ufupi:
Virutubishi mchanganyiko vinapotumiwa na watoto havileti madhara, lakini vinaweza kusababisha maudhi madogo madogo, mfano:
ØKuharisha kwa muda mfupi: Baadhi ya watoto hupata tatizo la kuharisha kwa muda mfupi baada ya kuanza kutumia virutubishi mchanganyiko. Hali hii hudumu
kwa kipindi kifupi tu kwani mtoto hurejea katika hali ya kawaida baada ya siku kadhaa. Inapojitokeza hali hiyo, mtoto anywe maji kwa wingi na aendelee kutumia chakula kilichoongezwa virutubishi mchanganyiko.
ØKupata choo cheusi: Hili ni jambo la kawaida na halina madhara yoyote. Rangi hii inatokana na uwepo wa madini chuma kwa wingi kwenye chakula kilichoongezwa virutubishi mchanganyiko.