Kwa ufupi:
Mradi wa uboreshaji wa mauzo, uhifadhi na ulaji wa nyama vijijini unafadhiliwa na Serikali ya Norway kupitia shirika lake la maendeleo (NORAD) chini ya mradi mkubwa wa Uhakika wa Chakula na Palo la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania (TARP 11 - SUA). Mradi huu unacndeshwa katika ukanda wa mashariki ya Tanzania katika mikoa ya Pwani na Morogoro. Watafiti wanatoka Chuo Kikuu cha Sokoinc
cha Kilimo na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula. Kwa kuanzia kuna vijiji vitatu vinavyoshiriki katika mradi huu; Chamakweza (Chalinze) katika mkoa wa Pwani, Mnjilili na Nyumbanhitu (Gairo) katika mkoa wa Morogoro.
Kijarida hiki kimeandaliwa ili kitumike katika uenezaji wa mbinu mbalimbali zinazohusika na mradi. Hizi ni pamoja na njia za maandalizi ya mwanzo, matayarisho (kukausha kwa kufukiza moshi na kutumia mionzi ya
jua) na kuhifadhi nyama iliyokaushwa.