Kwa ufupi:
Kampeni ya uhamasishaji wa elimu bora ya kilimo cha pamba umefanyika katika Wilaya ya Maswa lengo likiwa ni kuwaelimisha wakulima wa pamba kanuni bora za kilimo hicho ili waweze kulima kwa tija na kuongeza uchumi wa mkulima, wilaya na taifa kwa ujumla. Uhamasishaji huo umefanyika kwa siku 5 katika Wilaya ya Maswa.
Halmashauri ya wilaya ya maswa ina majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Maswa Mashariki na Maswa Magharibi yenye Kata 36, Vijiji 120 na Vitongoji 510 wakulima wa pamba katika Wilaya ya Maswa wapo zaidi ya 92,000 ambao kwa wastani wanalima heka 1 na kuendelea.
Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha Pamba kwa wingi hivyo kwa umuhimu huo serikali imeagiza Mkoa wa Simiyu kufikia 2025 iwe na uwezo wa kuzalisha Tani zipatazo 500,000 za pamba na Wilaya ya Maswa inatakiwa kuzalisha Tani 130,000 ifikapo mwaka 2025 kwa kuwa ni Wilaya ya pili kimkoa inayozalisha pamba kwa wingi. Ili kutilia mkazo katika zao hilo bodi ya pamba Tanzania chini ya balozi wake Mhe. Agrrey Mwanri imemlika katika Wilaya hiyo ya Maswa kuongeza nguvu kwa kutoa Elimu ya kanuni bora za kilimo cha pamba ambazo zitaongeza tija katika kilimo hicho na kumfanya mkulima kuzalisha kilo 2,000 kwa heka moja endapo atafata kanuni bora za kilimo cha kisasa cha zao la pamba ambalo litamwinua mkulima katika uchumi wake na kuongeza mapato ya Wilaya, mtu, kaya na familia kwa ujumla.