Kwa ufupi:
Chungwa ni tunda la mchungwa. Jina la kisayansi ni Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck kwenye familia ya Rutaceae.
Tunda lifahamikalo kisayansi kama Citrus sinesis huitwa chungwa tamu ili kutofautisha na Citrus aurantium, chungwa chungu.
Chungwa ni mahulusi kati ya pomelo (Citrus maxima) na chenza (Citrus reticulata). Mti wake mdogo utoao maua hufikia urefu takribani mita kumi na majani yake yasiyokauka muda wote.