Kwa ufupi:
Binzari ya manjano katika majiko ya nchi zote za Asia Kusini, ikiwa ni pamoja na India na Pakistan. Lakini je binzari manjono hutumiwa kwa ajili ya ladha ya chakula au inaweza kuboresha afya na kuzuwia saratani?
Utakuta maelfu ya makala zikielezea jinsi binzari ya manjano zinavyoweza kutibu magonjwa kama kiungulia, kukosekana kwa uwezo wa tumbo wa kusaga chakula, kisukari, huzuni na maradhi ya ubongo ya Alzheimer.Inaweze hata kuponya saratani. Maelfu ya tafiti yamekwishafanywa juu ya binzari ya manjano. Kiungo hiki kinasemekana kuwa na manufaa ya kimatibabu, na kiana kiungo kiitwacho curcumin.
Majaribio yaliyofanywa kwa panya yameonyesha kuzuia aina nyingi za saratani kukua ndani yake.
Lakini binzari manjano huwa na asilimia mbili hadi tatu za curcumin na tunapoila, miili yetu haifyonzi kiasi chote hicho. Hatahivyo, tafiti kuhusu binzari za manjano huripoti kwa nadra kiasi cha kawaida cha binzari hiyo katika mlo.
Kwahiyo ulaji wa kiasi kidogo cha Binzari ya manjano kunaweza kuboredha afya yetu au je tunapaswa kutumia virutubisho vya binzari ya manjano au curcumin kujikinga na magonwa.