Ghala la Mkulima

Utengenezaji na matumizi ya mboleavunde katika kilimo.

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.contributor.author Ngeze, Pius B
dc.date.accessioned 2024-02-23T07:13:03Z
dc.date.available 2024-02-23T07:13:03Z
dc.date.issued 1992
dc.identifier.isbn 978 9976 982 17 8
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/804
dc.description.abstract Mimca inapokuwa shambani hufyonza virutubisho vya mimea kutokaudongoni. Kali ya virutubisho hivyo, vilivyo muhimu zaidi ni nitrojeni, fosforasi, potasi, kalisi na feri. Mimea hutumia virutubisho hivyo kwa kukua, kuzaa, kujiimarisha na kupevusha matunda ili kutupatia mavuno yaliyo mengi na bora. Karibu sehemu zote za mimea zina virutubisho. Sehemu hizo ni mizizi, mashina,majani, maua na matunda. Lakini, si sehemu zote hizo hutumiwa na binadamu kwa chakula. Kwa kawaida sehemu zinazotumiwa ni maua, majani, mbegu matunda au tyuba. Hata hivyo, sehemu halisi inayotumika hutegemea aina ya zao au mmea. Sehemu zinazobaki ambazo hazitumiwi na binadamu au mifugo kwa chakula hubaki na virutubisho hivyo. Iwapo sehemu kama hizo zitaachwa ziharibike ovyo huko shambani, au kuzichoma moto, hasa nje ya shamba, aina hizo za vyakula zitapotea bure bila kuwafaidia wakulima wala taifa. Njia ya kuhakikisha kwamba masalia hayo ya mimea yanawafaidia wakulima ni kuyarudisha udongoni. Njia iliyo bora ya kufanya hivyo ni kuyaozesha masalia ya mimea na kuyatumia kutengeneza mboleavunde. Vivyo hivyo kwa masalia ya wanyama (hasa mifugo). Wanyama hula mimea. Kiasi cha chakula hicho hutumiwa na wanyama hao kwa kukua, kuzaa, kufanya kazi na kuishi. Kiasi kilichobaki hutolewa nje kama kinyesi. Kinyesi hicho kina virutubisho muhimu vya mimea. Njia nzuri ya kutumia kinyesi hicho cha mifugo ni kukitumia kutengeneza samadi na mboleavunde na kuziweka udongoni ili kustawisha mazao. Kufanya hivyo ni kudumisha uhai wa udongo na viumbehai vingine. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Tanzania Educational Publishers Ltd en_US
dc.subject Mboleavunde en_US
dc.subject Matumizi en_US
dc.subject Utengenezaji en_US
dc.subject Kilimo en_US
dc.title Utengenezaji na matumizi ya mboleavunde katika kilimo. en_US
dc.type Learning Object en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu