Kwa ufupi:
Kilimo shadidi cha mpunga (System of Rice Intensification—SRI) ni teknolojia bora yenye kutumia maji na mbegu kidogo kwa kutoa mavuno mengi. Hutumika kwa ku- badilishana kati ya kulowanisha kwa siku 3 na kukausha ardhi kwa siku 7 kwa kina cha sentimita 2 za maji yaliyotuama. Mu- da wa ukavu huweza kuwa kati ya siku 4 - 7. Mipasuko ya udongo kwenye jaruba ni kiashiria cha kumwagilia maji kwenye jaruba. Kama udongo ni wa mfinyanzi ta- hadhari kubwa yatakiwa kutoruhusu mipasuko ya kupitiliza kabla ya kum- wagilia ili kuepuka maji mengi kupotea isivyotarajiwa.