Ghala la Mkulima

Uanzishaji wa kitalu na ubebeshaji wa miche ya miembe

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.contributor.author Kusolwa, P.M,
dc.date.accessioned 2023-12-01T09:36:53Z
dc.date.available 2023-12-01T09:36:53Z
dc.date.issued 2023-11-14
dc.identifier.citation www.share4dev.info/kb/documents en_US
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/782
dc.description.abstract Kitalu ni mahali ambapo miche huoteshwa na kutunzwa kabla ya kupandikizwa kwenye bustani au shambani. Hii ni sehemu mama katika uzalishaji wa miche, na huchukua eneo dogo tu la shamba. Eneo hili ni muhimu kwa ajili ya uangalizi makini na urahisi wa huduma stahili kwa miche. Miche ya miembe hukaa kwenye kitalu hadi inapokuwa tayari kupandikizwa shambani au kuuzwa. Kubebesha miche (grafting) ni njia ya kitaalamu inayotumika kupandikiza mbegu kwa njia ya kitawi na kuunganisha mti au mmea wa jamii moja unaolingana sifa na tabia au wenye sifa na tabia tofauti ili kupata aina inayokusudiwa. Ubebeshaji hutumika pia katika uzalishaji wa miche ya aina mbalimbali za mboga (mfano nyanya), miti ya matunda na mapambo. Ili kubebesha au kuunganisha miche ya miembe kwa ufanisi, asili ya mche shina (rootstock) na aina ya tawi (scion) sifa zake ni vema zijulikane. Sifa hizi ni pamoja na uzaaji wa matunda mengi bora na ustahimilivu wa magonjwa. Pia, ni muhimu kuchagua aina ya miembe inayopendwa na walaji au inayohitajika kwenye soko. Sababu kuu ya kubebesha miche ya miembe ni kuharakisha muda wa uzaaji ambao ni kati ya miaka mitatu hadi mitano badala ya miaka 7 mpaka 8 kwa miembe ya kienyeji ambayo haikubebeshwa mfano embe Nyonyo, Dodo, Kitanga, Ngwangwa na Sindano. Pia mche uliounganishwa unadumisha au unaendeleza sifa halisi za mmea mama ambao kikonyo chake kimetumika kwenye kuunganisha. Vilevile, kuunganisha mche kunatoa nafasi ya kutumia mimea shina ambayo ina uwezo, kwa mfano; kuvumilia ukame, magonjwa na hali ya udongo ambayo mmea tawi usingeweza kuvumilia. Katika kijitabu hiki tutajifunza kuhusu uanzishaji kitalu, aina za vitalu, sifa za eneo la kuanzisha kitalu, ubebeshaji wa miche ya miembe, udhibiti wa mizizi ya miche itarajiwayo kubebeshwa kitaluni, kubebesha au kuunganisha miche, kuchagua vitawi au vikonyo kwa ajili ya kubebesha miembe, sifa za mti mama wa mmea shina, muda na mazingira mazuri ya kubebesha miche ya miembe, hatua za kubebesha miche ya miembe na vifaa vinavyotumika kubebeshea. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Kituo cha utafiti wa kilimo en_US
dc.subject Miembe en_US
dc.subject Kitalu en_US
dc.subject Ubebeshaji wa miche en_US
dc.title Uanzishaji wa kitalu na ubebeshaji wa miche ya miembe en_US
dc.title.alternative Sifa za eneo la kuanzisha kitalu en_US
dc.type Learning Object en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu