Kwa ufupi:
Mbili-Mbili ni mkakati wa kilimo mseto cha nafaka na mikunde unaohusishaupandaji wa mazao matatu yenye ukuaji na mpangilio tofauti shambani. Tekinolojia hii ilitengenezwa kwa mfumo wa utafiti wa Afrika katika uimarishaji maendeleo endelevu kwa kizazi kijacho. Mradi wa Africa RISING umelenga kuwasaidia wakulima wadogowadogo kuondokana na njaa, uhaba wa chakula, utapiamlo na umaskini. Hapo awali, kazi kubwa ilifanyika kukuza mazoea ya matumizi ya mbinu bora za kilimo kama vile mchanganyiko wa mbinu za utunzaji rutuba ya udongo (ISFM) ambazo zimeongeza tija ya mahindi kwa mafanikio mazuri. Ingawa, tija ya mikunde imebaki kuwa ndogo, mfano uzalishaji wa maharage ni chini ya kilo 250 na mbaazi ni chini ya kilo 400 kwa hekta. Kwa kutambua hilo, shirika la Kimataifa la Kilimo cha Kitropiki (International Centre for Tropical Agriculture (CIAT)) ambalo ni mojawapo ya mashirika yanayohusika katika kutekeleza mradi wa Africa RISING, limeanzisha na kuthibitisha mitindo ya kulima mikunde, Mbili-Mbili ikiwa mojawapo, katika wilaya ya Babati, Tanzania. Mbili-Mbili huhusisha kutumia nafasi za mimea kuongeza upenyaji wa mwanga wa jua kwenye mikunde, isipofanyika hivyo, mara nyingi mikunde hufunikwa na kivuli cha mazao ya nafaka kama mahindi. Lengo muhimu ni kuongeza tija ya mbaazi na maharage huku tukidumisha tija sawa ya mahindi. Tekinolojia ya Mbili-Mbili ina faida ya ukuaji haraka, wa kati na wa muda mrefu wa maharage, mahindi na mbaazi kwa pamoja ambayo hupunguza ushindani wa rutuba, unyevu na mwanga kati ya mazao haya matatu. Mazao mengine yoyote yanaweza kutumika ikiwa tu yana mifumo ya ukuaji isiyo athiriana. Jina Mbili-Mbili limetokana na neno la Kiswahili “Mbili”. Katika Mbili-Mbili mistari miwili ya mahindi hupishana na mistari ya aina mbili za jamii ya mikunde (mchoro 1). Tekinolojia hii ilifanyiwa