Ghala la Mkulima

Tathmini ya asali za kiangazi katika mabonde a mpunga

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.contributor.author Wizara ya Kilimo
dc.date.accessioned 2023-10-05T10:18:16Z
dc.date.available 2023-10-05T10:18:16Z
dc.date.issued 2011-03
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/756
dc.description.abstract Ndugu Wakulima; sote tunakubaliana kwamba kilimo cha umwagiliaji maji ndio mkombozi wetu kwa ukulima wa mpunga, umuhimu wake umezidi kuwa mkubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa yanayotokea duniani kote, hali inayosababisha kilimo cha kutegemea mvua kutokuwa cha uhakika na cha matumaini. Hivyo, tunahitaji kujipanga vyema na kukiimarisha kilimo cha umwagiliaji maji ili tuwe na uhakika wa chakula na kupunguza uagizaji. Kwa mujibu wa Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji wa mwaka 2003, Zanzibar tunalo eneo la ekari 21,300 ambazo zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji maji. Hadi sasa eneo lililojengwa miundombinu ni ekari 1,750 sawa na asilimia 8% tu ya eneo lote. Eneo lililobaki lenye ukubwa wa ekari 19,550 kati ya hizo ekari 200 zimejengwa makinga maji, ekari zilizobaki 19,350 zinaendelea kutumika kwa uzalishaji wa mpunga wa kutegemea mvua. Ndugu Wakulima pamoja na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu, bado tunakabiliwa na changamoto za gharama kubwa za ujenzi wa miundombinu, ukarabati wa visima na pampu kutokana na teknolojia duni upungufu wa wataalamu na elimu ya uendeshaji wa jumuiya za wakulima na upungufu mkubwa wa mitaji, utegemezi mkubwa wa nishati ya umeme, uharibifu wa vianzio vya maji pamoja na ukosefu wa zana maalum za utayarishaji wa ardhi. Kutokana na changamoto hizo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya eneo linalofaa kwa umwagiliaji maji linalimwa kwa kutegemea mvua hali ambayo inapelekea uzalishaji na tija ndogo. Ndugu Wakulima, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo 2011 – 2016 Wizara ya Kilimo na Maliasili imekusudia kuutekeleza kikamilifu Mpango Mkuu wa Umwagiliaji maji ambao unatarajiwa kutatua changamoto zote za kilimo hicho. Wizara imezungumza na Serikali ya Korea kupitia Benki ya EXIM – ambao wamekamilisha uhakiki wa eneo la ekari 5250 ambalo litajengwa mindombinu ya umwagiliaji maji. Serikali ya Japan na Benki ya BADEA pia wameonesha nia ya kutusaidia katika Kilimo cha umwagiliaji maji. Ndugu Wakulima, Wizara imekusudia kuendeleza ujenzi wa miundombinu na utunzaji wa vianzio vya maji ili sekta ya umwagiliaji maji ipate maendeleo endelevu na kuwawezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga. Kuzijengea uwezo Jumuiya za Wakulima wa umwagiliaji maji ziweze kushiriki kikamilifu katika uendeshaji na utunzaji wa miundombinu, uhifadhi wa vianzio vya maji na utoaji wa huduma za Kilimo. Wizara inaendelea kuwashajihisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuchagua miradi ya kijamii ya umwagiliaji maji ikiwemo ujenzi wa miundombinu na makinga maji kila wanapopata fursa ya usaidizi wa Washirika wa Maendeleo. Ndugu Wakulima, napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa wakulima wa mpunga wa umwagiliaji maji watumie mbegu bora na pembejeo zinazotolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo na kuhakikisha kuwa miundombinu ya umwagiliaji maji iliyojengwa kwa gharama kubwa tunaitumia kikamilifu katika uzaalishaji wa zao hili. en_US
dc.publisher Wizara ya Kilimo Srikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Zanzibar en_US
dc.relation.ispartofseries ;5
dc.subject Mpunga en_US
dc.subject Kiangazi en_US
dc.title Tathmini ya asali za kiangazi katika mabonde a mpunga en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu