Kwa ufupi:
Kitabu hiki Jifunze Ufugaji Bora wa Samaki Aina ya Sato na Kambale kimeandikwa kutokana na uhaba mkubwa tulionao nchini wa majarida na vitabu vyenye lengo la kumsaidia Mtanzania kuongezaupatikanaji wa chakula na kukuza kipato. Mara nyingi vitabu vinavyoandikwa zaidi nchini vinahusu utamaduni wa Mtanzania;aghalabu hadithi, nyimbo, historia mbali mbali na vingine vinalenga ukulima wa mazao mbali mbali kama mahindi, mihogo n.k. Aidha, hakuna machapisho ya kutosha yaliyo kwa lugha ya Kiswahili ili kumsaidia mkulima wa kitanzania kuelewa vema mbinu bora za ufugaji samaki.Kwa mantiki hii, kitabu hiki kimeelezeakwa lugha nyepesi ya Kiswahili kanuni za ufugaji bora wa samaki kwa kuzingatia mbinu na teknolojia sahihi za ufugaji bora wa samaki aina ya Sato (au perege kama wengine wanavyomwita) na kambale ili kuwa na ufugaji endelevu. Kanuni hizi zinalenga kupanua uelewa wa wadau katika uhudumiaji, usafirishaji na uhifadhi wa samaki na mazao yake.