Kwa ufupi:
Tumbaku huzalishwa kwa ajili ya majani yake,majani ya tumbaku yanapo komaa
huvunwa na tumbaku hutumika hasa kutengeneza sigara.Aina za tumbaku zinazo limwa Tanzania ni tumbaku ya mvuke (VFC) na tumbaku ya moshi (DFC). Tumbaku ya Moshi hulimwa kusini mwa Tanzania hasa Ruvuma na tumbaku ya Mvuke hulimwa Tabora,
Shinyanga, Kigoma, Katavi, Iringa, Mbeya, Songwe, Singida, Morogoro, Mara, Kagera
na Geita.