Kwa ufupi:
Malisho ni chakula cha msingi cha mifugo
kinachojumuisha aina mbalimbali za nyasi na
mikunde. Utunzaji wa malisho ni muhimu ili
kuhakikisha kwamba mifugo inapata chakula
bora na cha kutosha wakati wote. Ukuaji na
ustawi wa aina za malisho hutofautiana
kutegemea hali ya hewa na mazingira
mbalimbali.
USTAWISHAJI WA MALISHO
• Andaa shamba.
• Chagua aina ya malisho unayokusudia
kupanda kufuatana na aina ya
udongo na hali ya hewa.
• Panda mbegu bora kufuatana na aina
ya malisho (mbegu, vipingili, vishina
au chipukizi). Mbegu bora zipandwe
kwa ekari kilo 5-10 kwa nyasi na kilo
2-6 kwa mikunde kutegemea aina ya
mbegu.
• Ondoa magugu kupunguza ushindani
wa maji, hewa na mwanga kati ya
malisho na magugu.
• Weka mbolea ya samadi, mboji au ya
viwanda kama NPK, CAN, TSP kwa
kufuata ushauri wa mtalaamu wa
mifugo.
• Hakikisha malisho yanapata maji ya
kutosha