Kwa ufupi:
Mwani ni aina ya mimea inayoota na kukua
kwenye maji chumvi (bahari) na maji baridi
(mito, maziwa na mabwawa). Tofauti iliyopo
kati ya mwani na mimea mingine inayokua
kwenye nchi kavu ni kwamba mwani
hautegemei mizizi kufyonza maji na
virutubisho vingine bali hutumia sehemu
zote za mmea kuvyonza virutubisho
vinavohitajika kutoka kwenye maji. Aina ya
jamii ya mwani inayolimwa nchini Tanzania
kitaalam hujulikana kama “Eucheuma
denticulatum” na pia huitwa Eucheuma
spinosum. Aina nyingine ni “Kappaphycus
alvarezii” kwa jina jingine Eucheuma
cottonii.