Kwa ufupi:
Soya (Glycine max) ni zao la jamii ya mikunde. Zao hilo asili yakeGlycine max) ni zao la jamii ya mikunde. Zao hilo asili yakeGlycine max
ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800
iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907
katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya miaka ya 1930
na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya
Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na
Peramiho mkoa wa Ruvuma. Kuenea kwa zao hilo katika maeneo
hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas Food
Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General
Agricultural Production for Export – (GAPEX) naAgricultural Production for Export – (GAPEX) naAgricultural Production for Export National Milling
Corporation – (NMC). Mashirika hayo yalisafirisha soya kwenda
katika nchi za Japan na Singapore.
Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko
la nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu
hiyo baada ya mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo
cha soya kilififia hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni
mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena baada ya jamii
kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza
vyakula vya watoto