Kwa ufupi:
Uwele (Panicum miliaceum) ni nafaka na mbegu ndogo. Una virutubisho kwa wingi, ukiwa ni chanzo kizuri cha vitamin B na madini chuma. Unahusiana na mtama. Lakini una protini na nyuzinyuzi nyingi zaidi ya mahindi.
Katika Marekani na nchi nyingine tajiri, uwele unatumika sana kwa ajili ya chakula kuku na mbegu za ndege. Katika Africa, Asia, kaskazini ya China na sehemu nyingine za dunia, uwele ni chakula kikuu cha kila siku.