Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uhakika wa Chakula, pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH),
kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania. Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya Wakulima, Watafiti na Washauri wa Ugani. IIi kufikia lengo hili, mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda. Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara mbili (kanda moja kwenda kanda nyingine) zilizofanyika mwezi Agosti na Septemba 2001. Ziara ya kwanza ya kimafunzo ya wakulima iliwashirikisha wakulima na washauri wa ugani kutoka wilaya za Mbinga, Njombe, Makete na Mbeya (Kanda ya nyanda za juu kusini) hawa waliwatembelea wakulima wenzao wa wilaya ya Lushoto. Ziara ya pili iliwajumuisha wakulima na washauri wa ugani kutoka
wilaya za Bagamoyo, Morogoro Vijijini na Kilosa (Kanda ya Mashariki) ambao waliwatembelea wakulima wa wilaya za Njombe na Mbarali.