xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.date.accessioned | 2019-07-24T05:49:07Z | |
dc.date.available | 2019-07-24T05:49:07Z | |
dc.date.issued | 2008 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/handle/123/490 | |
dc.description.abstract | Kwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa kuku mwenyewe. Hivyo ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige kuku anavyofanya. Ikumbukwe kuwa vifaranga husumbuliwa zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa na kukosa uangalizi wa karibu. Ni lazima vifaranga waangaliwe kwa kuwapatia nyumba yenye joto, chakula kinachofaa na maji safi , kuwakinga dhidi ya magonjwa masumbufu kwenye eneo husika na kuwatibu wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri ambao hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida. Wafugaji wengi vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga vifaranga wake kwa muda mrefu hadi wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku kurudia kutaga na hivyo kupata vifaranga wachache zaidi kwa mwaka. Lakini vifaranga vikiondolewa kwa kuku mapema, kama majuma matano hivi baada ya kuanguliwa, na wakatunzwa na mfugaji, kuku hutaga mapema na idadi ya kuku kwa mfugaji huongezeka haraka ndani ya kipindi kifupi. Mwongozo huu unaeleza jinsi ya kufuga vifaranga vizuri ili hatimaye mfugaji apate faida zaidi. | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | Rural Livelhood Development Company - RLDC | en_US |
dc.subject | Kuku | en_US |
dc.subject | Vifaranga | en_US |
dc.subject | Ufugaji | en_US |
dc.title | Kulea vifaranga: Mwongozo kwa Mfugaji siku 1 hadi wiki 5 | en_US |
dc.type | Article | en_US |