xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.date.accessioned | 2019-02-18T07:25:23Z | |
dc.date.available | 2019-02-18T07:25:23Z | |
dc.date.issued | 2006-12 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/handle/123/435 | |
dc.description.abstract | Sekta ya Mifugo ina nafasi kubwa katika kujenga uchumi imara wa Taifa, kuongeza kipato kwa Watanzania wanaotegemea mifugo, na kutoa fursa za ajira sanjari na kuhifadhi rasilimali za Taifa. Sera hii inaeleza nia ya Serikali na wadau wengine katika kukabiliana na changamoto zinazokabili Sekta ya Mifugo. Jukumu kubwa ni kujenga mazingira mazuri yatakayotoa fursa za kuongeza kipato na ajira kwa wafugaji wadogo, kufuga kibiashara na kuongeza ajira. Ili kufikia haya, malengo makuu matatu ya kisera yatatekelezwa kama ifuatavyo:- • Kuendeleza Sekta ya Mifugo itakayokuwa na mwelekeo wa kibiashara, yenye ufanisi na itakayohimili ushindani wa kimataifa; • Kuibua mifumo bora ya uzalishaji itakayoongeza tija miongoni mwa wafugaji wadogo; na • Kuhifadhi rasilimali za mifugo na kuunda sera na taasisi zitakazosimamia maendeleo na matumizi endelevu ya rasilimali hizo. Mabadiliko yanayotarajiwa katika Sekta ya Mifugo ni sehemu ya mchakato mzima wa kuleta maendeleo vijijini ambayo ni pamoja na Programu ya Kuboresha Serikali za Mitaa, umilikishaji wa ardhi kwa wananchi, uwekezaji katika miundombinu na utoaji wa huduma bora za jamii. Marekebisho haya yanalenga kuchangia katika kutekeleza Dira ya Maendeleo Tanzania 2025 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA). Aidha, mafanikio katika Sekta ya Mifugo, yatategemea ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kupunguza umaskini. | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | Wizar ya Maendeleo ya Mifugo - Tanzania | en_US |
dc.subject | Sera | en_US |
dc.subject | Mifugo | en_US |
dc.title | Sra ya Taifa ya Mifugo | en_US |
dc.type | Book | en_US |