Kwa ufupi:
Kati kati ya mwaka 2002, wakulima 1128 waliokuwa wakiishi sehemu ya kaskazini mashariki ya Tanzania, kwenye miteremko mikali ya milima ya Usambara Mashariki, waliambiwa kwamba mazao katika mashamba yao madogomadogo katika misitu, nje ya vijiji vyao ilibidi yafyekwe ili kuihifadhi misitu hiyo. “Ushoroba Mpya wa Derema” utakuwa ni kiungo kati ya hifadhi mbili za misitu ambayo inalindwa na mwendelezo wa makazi ya mamia ya ndege, wanyama watambaao, wadudu, spishi za wadudu na mimea ambayo ni adimu sana, na mingine ambayo inatishiwa kutoweka. Wakulima walilipwa fidia ya mazao ambayo yalikuwa katika mpaka wenye upana wa mita tatu kuzunguka ushoroba; mpaka ambao uliwekwa kwa kufyeka mimea iliyokuwa katika mpaka huo. Mazao yao ndani mpaka –yenye thamani kubwa, yale ya iliki, mdalasini, karafuu na pilipili manga, pamoja na baadhi ya miti ya matunda – yalihesabiwa na kuorodheshwa kwa ajili ya kulipiwa fidia baadaye.