Kwa ufupi:
Ufugaji wa Nguruwe ni kati ya shughuli zinazokuwa haraka katika Afrika Mashariki na ya Kusini. Ukuaji wa miji na ongezeko la watu kumeendana na ongezeko kubwa la mahitaji ya protini ya wanyama. Uwezo wa kukua haraka, ubora wa nyama kiafya na ladha nzuri inatoa nafasi kubwa ya maendeleo ya ufugaji wa nguruwe kama chanzo cha kipato kwa mfugaji. Kijarida hiki kinatoa mwongozo kuhusu mahitaji muhimu ya ufugaji nguruwe, mbinu za kuboresha uzalishaji, kudhibiti magonjwa na pia mwongozo wa kujali haki za nguruwe kama kiumbe hai kinachoweza kusikia maumivu kisipotendewa kinavyostahili. Nguruwe ana gharama ndogo za matunzo, anatoa mafuta, huleta kipato cha pesa, hutoa mbolea ya mimea. Faida ya ufugaji nguruwe hutegemea zaidi ubora wa matunzo. Vile vile kumbuka kutumia vyanzo nafuu vya chakula na kujengea miudombinu. Msomaji anashauriwa kuwaona wataalamu kwa ushauri zaidi na pia kusoma vitabu vya rejea kuhusu ufugaji nguruwe