Kwa ufupi:
Saratani (Cancer) ni ugonjwa unaotokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo
wake wa kugawanyika na hivyo hazipo katika hali yake ya kawaida. Seli hizo
huweza kugawanyika bila mpangilio maalum na kuharibu mkusanyiko wa
seli nyingine. Seli za saratani hutokea sehemu moja ya mwili na zinaweza
kusambaa sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu na limfu
(lymph). Saratani inaweza kuwa ya kurithi au kusababishwa na hali ya
mazingira ya vitu mbalimbali kama vile ulaji wa vyakula vyenye visababisha
saratani (carcinogenic compounds), km. nyama iliyochomwa mpaka kuungua
kidogo, ulaji usio bora, pombe, uvutaji sigara au mionzi hatari, aina ya madini
kama “asbestos” na “lead”. Zipo pia baadhi ya saratani zinazosababishwa
na virusi kama vile saratani ya shingo ya kizazi.