Kwa ufupi:
Kufuatia kukamilika kwa Awamu ya Uandaaji wa Maboresho Julai 2008,
MKURABITA iliingia katika awamu yake ya Tatu ambayo ni Utekelezaji wa
Maboresho. Menejimenti ya MKURABITA ilianza kwa kutekeleza baadhi ya
mapendekezo hayo yanayo husiana na urasimishaji wa rasilimali vijijini na hata
mijini kwa utaratibu iliyoita “FRONT RUNNERS” kwa mbinu ya Ujengeaji uwezo
Halmashauri za wilaya. Katika utaratibu huu MKURABITA ilianza na wilaya kumi
ambazo ni Makete, Njombe, Wete, Musoma, Serengeti, Manyoni, Mpwapwa,
Mvomero, Rufiji na Nachingwea.