Kwa ufupi:
Samaki wamekuwa ni chanzo kizuri na kikubwa cha protein Duniani. Ulaji wa samaki
umeongezeka maradufu tokea Mwaka 1973; asilimia 90 (90%) la ongezeko hilo likiwa kwa
nchi zinazoendelea (Developing Countries). Tani milioni 45.4 za samaki zililiwa Duniani
Mwaka 1973: India-tani milioni 1.8, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara-tani milioni 2.6;
China-tani milioni 4.9 na Japan-tani milioni 7.6. Benki ya Dunia (WB) inakadiria kwamba
ifikapo Mwaka 2030, asilimia 70 (70%) ya mahitaji (matumizi/ulaji) ya samaki yatatokea
kwenye Bara la Asia.