Ghala la Mkulima

Watu na nyuki: Mwongozo (kwa lugha nyepesi) wa Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.date.accessioned 2018-06-13T08:09:21Z
dc.date.available 2018-06-13T08:09:21Z
dc.date.issued 2004-08
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/handle/123/150
dc.description.abstract Kijitabu hiki kunatoa mwongozo kwa lugha nyepesi kuhusu Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki Tanzania inayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2001–2010. Programu hii iliidhinishwa na Serikali mwezi Novemba 2001. Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki (PTUN) inakidhi mahitaji ya jumla ya mpango wa maendeleo nchini, hasa Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKU). PTUN imeundwa kutokana na mawazo makuu au misingi inayohusiana na maendeleo endelevu na Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Nyuki (UERN). Hii ina maana kwamba mipango ya maendeleo lazima ipangwe kwa kushughulikia masuala ya mazingira, jamii na uchumi. Kama uchumi utakua wakati mazingira yanaharibika na watu wengi wanakuwa maskini, maendeleo hayatakuwa endelevu. Kwa hivyo PTUN inalenga katika uhifadhi wa mazingira, ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini kwa wakati mmoja. Kama uchumi utakua wakati mazingira yanaharibika na watu wengi wanakuwa maskini, maendeleo hayatakuwa endelevu Mtazamo wa PTUN unahusisha mabadiliko ya Sera za Serikali yanayohimiza ushirikishwaji wa jamii, sekta binafsi, washirika katika maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vya ufugaji nyuki na vyama mbalimbali katika usimamizi wa rasilimali za nyuki. Ushiriki sawa wa wanawake na wanaume utahimizwa na hii itasaidia katika maendeleo ya uchumi na kupunguza umaskini. Huu ni mtazamo thabiti na wa kusisimua ambao unaleta changamoto na manufaa mengi.Yote haya yamefafanuliwa katika kijitabu hiki. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Wizara ya Maliasili na Utalii en_US
dc.subject Nyuki en_US
dc.subject Mwongozo en_US
dc.subject Asali en_US
dc.title Watu na nyuki: Mwongozo (kwa lugha nyepesi) wa Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania en_US
dc.type Book en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu