Kwa ufupi:
Kijitabu hiki kunatoa mwongozo kwa lugha nyepesi kuhusu Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki
Tanzania inayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2001–2010. Programu hii iliidhinishwa na Serikali
mwezi Novemba 2001.
Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki (PTUN) inakidhi mahitaji ya jumla ya
mpango wa maendeleo nchini, hasa Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKU).
PTUN imeundwa kutokana na mawazo makuu au misingi inayohusiana na
maendeleo endelevu na Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Nyuki (UERN).
Hii ina maana kwamba mipango ya maendeleo lazima ipangwe kwa
kushughulikia masuala ya mazingira, jamii na uchumi. Kama uchumi utakua
wakati mazingira yanaharibika na watu wengi wanakuwa maskini, maendeleo
hayatakuwa endelevu. Kwa hivyo PTUN inalenga katika uhifadhi wa
mazingira, ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini kwa wakati mmoja.
Kama uchumi utakua
wakati
mazingira
yanaharibika na watu
wengi
wanakuwa
maskini, maendeleo
hayatakuwa endelevu
Mtazamo wa PTUN unahusisha mabadiliko ya Sera za Serikali yanayohimiza ushirikishwaji wa jamii,
sekta binafsi, washirika katika maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vya ufugaji nyuki na
vyama mbalimbali katika usimamizi wa rasilimali za nyuki. Ushiriki sawa wa wanawake na wanaume
utahimizwa na hii itasaidia katika maendeleo ya uchumi na kupunguza umaskini.
Huu ni mtazamo thabiti na wa kusisimua ambao unaleta changamoto na manufaa mengi.Yote haya
yamefafanuliwa katika kijitabu hiki.