Kwa ufupi:
Utoaji wa makala hii ni sehemu ya mradi wa ushirikiano baina ya CIALCA na MtandaoAfya
(HealthNet) TPO ujulikanayo kama “destuli endelevu za kilimo na afya kwa uimalishaji lishe
na afya kwa jamii ndogondogo nchini Burundi (upande wa afya Kanda ya Gitera) na Jamhuri
ya Demokrasia ya Kongo- DR Congo (upande wa afya Kanda ya Butembo). Makala hii
imekusudiwa kutumika na wataalam kilimo, wachumi wa masuala ya nyumabani, wataalam
lishe, na watumishi wa afya katika kuwajengea uwezo wawezeshaji katika jamii husika
(community own resource persons) (CORPs). Matarajio kwa ujumla ni kuimalisha kiwango
cha lishe miongoni mwa wanajamii kupitia destuli sahihi za ulaji na mikakati endelevu ya
kilimo.
Maudhui yaliyomo katika makala hii yalichambuliwa kufuatia mapungufu yaliyoonekana
katika ngazi ya jamii kupitia mahojiano ya vikundi na mapitio ya kaya. Mwongozo huu
kwanza unaelezea mlolongo unaojumuisha kilimo, lishe na afya. Halafu, unatoa elimu ya
msingi ya lishe juu ya aina za virutubishi na vyanzo vyake katika maeneo husika.