Kwa ufupi:
Mti wa mwarobaini unayo matumizi na faida nyingi, lakini hapa tutajadili umuhimu wa mti
huu katika kuzuia na kukabili wadudu na magonjwa ya mimea. Duniani kote, theluthi moja
ya vyakula vilivyo shambani au kuhifadhiwa hupotezwa kwa kuvamiwa na wadudu kila
mwaka. Mpunga na mahindi ndio huadhiriwa kwa wingi katika Afrika na Asia. Lengo kuu la
makala haya ni kueleza jinsi mwarobaini unavyoweza kutumiwa katika kukabili shida hii.