Kwa ufupi:
Nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa mfano, zimejaliwa raslimali ambazo zinaweza kub-
adilishwa kuwa mali. Lakini suala ni jinsi ya kuzigeuza raslimali hizo ili kuwa vitu halisi. Elimu isiyofaa
imeelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa kinachokwamisha kuzibadilisha raslimali hizo kuwa vitu halisi.
Elimu ya Tanzania inasemekana kuwa ni elimu inayowaandaa watu kuwa waajiriwa wa maofsini, japokuwa
nafasi za kazi ni chache ukilinganisha na idadi ya watu wanaotafuta kazi za kuajiriwa. Kwa ufupi, elimu
yetu haijengi ubunifu na udadisi ambao ungewawezesha watu ama kujiajiri (ujasiriamali) au kuzipanua
fursa za ajira ambazo zingewawezesha watu wengi kupata ajira. Fursa za ajira hazijatumiwa kwa kiwango
kikubwa kiasi cha kuweza kuwachukua watu wote wenye sifa za kuajiriwa. Chapisho hili kwa hiyo linaibua
jinsi elimu ya ujasiriamali inavyoweza kuibadilisha nchi kutoka kwenye utegemezi na kuwa nchi yenye
kujitegemea.