Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeteke1eza tafiti zilizofadhiliwa na Serikali ya Norway kupitia shirika 1ao la NORAD kuanzia na TAN 90, TAN 20 na TARP - SUA, FOCAL na mwishowe PANTIL. Mradi wa PANTIL una lengo la kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mafunzo kwa vitendo, utafiti, na ushauri. Mradi pia unalenga katika kujenga misingi imara ya utafiti na ushauri kilimo na maliasili inayokidhi mahitaji ya jamii za wakulima na kutoa fursa mpya kwao. Aidha, mradi unatilia mkazo, mbinu fungamanishi ya nyanja anuai na maisha endelevu itakayosaidia walengwa kunufaika na huduma zaidi ya tekinolojia ya kilimo na ufugaji bora.