Kwa ufupi:
PELUM Tanzania ni mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yanayofanya kazi na wakulima na wafugaji wadogo nchini Tanzania. Mtandao
huu ulianzishwa mwaka 1995 na kusajiliwa kisheria mwaka 2002. Kazi kuu
ya PELUM Tanzania ni kuhamasisha na kuendeleza kilimo endelevu kwa
kujenga uwezo wa Mashirika Wanachama kwa njia ya kutandaa, kutunza
na kueneza habari pamoja na ushawishi na utetezi. Walengwa wakuu wa
PELUM Tanzania ni Mashirika Wanachama ambapo wanufaikaji ni wakulima
na wafugaji wadogo wanaohudumiwa na Mashirika Wanachama. Kwa sasa
mtandao huu unaundwa na Mashirika Wanachama 33 yanayohudumia
wakulima na wafugaji wadogo zaidi ya milioni moja na laki mbili katika
mikoa 16 ya Tanzania Bara.